Rais Xi ataka mfumo uboreshwe ili kupiga hatua kubwa za kiteknolojia kwenye maeneo muhimu
2022-09-07 08:40:47| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuboreshwa kwa mfumo mpya wa kuhamasisha raslimali za nchi kutimiza maendeleo makubwa ya teknolojia kuu kwenye maeneo muhimu, na kuimarisha kwa pande zote juhudi za kuhifadhi raslimali.

Rais Xi ametoa kauli hiyo alipoongoza mkutano wa 27 wa Kamisheni Kuu ya Kuimarisha Mageuzi Kwa Pande Zote.

Rais Xi ambaye pia ni mkuu wa kamisheni hiyo, amesema China inapaswa kutumia vyema manufaa ya Usoshalisti ambao una uwezo wa kuhamasisha raslimali kwa ajili ya kukamilisha mipango mikuu, kuimarisha uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali kwenye uvumbuzi muhimu wa sayansi na teknolojia, na kutoa nafasi kamili kwa soko.