China yampongeza Bw. Ruto kuchaguliwa kuwa rais wa Kenya
2022-09-07 08:30:05| CRI

China imempongeza makamu wa rais wa Kenya Bw. William Ruto kuchaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning leo hapa Beijing amesema, China inatumai kuwa Kenya itadumisha amani na utulivu na kupata maendeleo makubwa zaidi. Amesema Kenya ni mwenzi muhimu wa ushirikiano wa China katika kanda ya Afrika Mashariki, na China inapenda kushirikiana na Kenya ili kusukuma mbele zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati yao.