China na Rwanda zarefusha makubaliano ya ushirikiano wa kimatibabu kwa miaka mingine mitano
2022-09-09 09:12:23| CRI

Wizara ya Afya ya Rwanda na Ubalozi wa China nchini humo wamesaini hati ya maelewano ya kurahisisha utumaji wa wafanyakazi wa afya wa China nchini Rwanda.

Akiongea kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika Jumatano mjini Kigali waziri wa afya wa Rwanda Bw. Daniel Ngamije, amesema wanatarajia ujio wa madaktari wa China kutoka vitengo ambavyo Rwanda inakosa wataalamu. Amesema Rwanda inashukuru ushirikiano huo uliodumu kwa miaka 40, na pia inawashukuru madaktari wa China waliotoa na wanaotoa huduma nzuri nchini Rwanda.

Balozi wa China nchini Rwanda Wang Xuekun amesema China na Rwanda zina urafiki wa muda mrefu, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye nyanja ya matibabu na huduma za afya, unaonesha urafiki wa kweli katika dhiki na faraja kati ya nchi hizo mbili.