UN: Shehena ya kwanza ya msaada wa kibinadamu wa nafaka kutoka Ukraine yawasili Ethiopia
2022-09-09 09:36:20| CRI

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema shehena ya kwanza ya msaada wa kibinadamu wa nafaka kutoka Ukraine kupitia Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) imewasili Ethiopia na inatarajiwa kukidhi mahitaji ya mwezi mmoja kwa watu zaidi ya milioni 1.5 waliokimbia ukame na migogoro.

Amesema utulivu wa minyororo ya ugavi ni muhimu kwa operesheni za WFP ambapo watu milioni 20 nchini humo wanahitaji msaada wa chakula. Lakini hadi sasa hakuna msafara wa kibinadamu unaoweza kufika Tigray tangu wiki mbili zilizopita, na safari za ndege za kila wiki za kusafirisha misaada ya kibinadamu kati ya Addis Ababa na Mekelle pia zimesitishwa.