Rais Xi atoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza
2022-09-09 15:01:20| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa salamu za rambirambi kwa mfalme mpya wa Uingereza, Charles III kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II.

Kwenye salamu zake, rais Xi amesema Malkia Elizabeth II akiwa kiongozi aliyetawala Uingereza kwa muda mrefu zaidi amepata sifa nzuri sana. Malkia Elizabeth II alikuwa mtawala wa kwanza wa Uingereza kufanya ziara nchini China. Kifo chake ni pigo kubwa sana kwa watu wa Uingereza.

Rais Xi amesisitiza kuwa anazingatia sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Uingereza na anapenda kushirikiana na mfalme Charles III na kutumia fursa ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya mabalozi na kusukuma mbele maendeleo mazuri ya uhusiano wa pande mbili ili kunufaisha nchi hizi na watu wake.

Wakati huohuo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Uingereza Liz Truss kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II.