Tamasha la Mitindo la Afrika laibua vipaji vipya
2022-09-12 08:30:21| CRI

Tamasha la 14 la Mitindo ya Afrika Duniani la mwaka 2022 (FESMMA) limemalizika Jumamosi jioni, ambapo zaidi ya wabunifu wa mitindo 20 walishiriki kwenye tukio hilo lililofanyika kwa siku nne huko Catonou nchini Benin.

Mwanamitindo wa Togo Assiata Adeola, mwenye miaka 20, ambaye alitumia nyuzi kutengeneza mkusanyiko wake ulioitwa “Usanifu”, alishinda taji la mbunifu bora wa mitindo Afrika siku ya Jumamosi, baada ya onesho kubwa la mitindo lililofanyika mwisho wa tamasha. Naye Kindo Ba Faridatou kutoka Burkina Faso alishinda tuzo ya mwanamitindo bora.

Wakati wa onesho hilo la mitindo lililofanyika kwa saa nne, wanamitindo walionesha umahiri na ubinifu wa wabunifu wa mitindo kutoka Afrika, Asia na Ufaransa katika kushona vitambaa vilivyotengezwa barani Afrika.