Rais wa China kuhudhuria mkutano wa SCO na kufanya ziara nchini Kazakhstan na Uzbekistan
2022-09-12 15:32:33| CRI


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema, kuanzia tarehe 14 hadi 16 Septemba, rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano wa 22 wa Kamati ya Viongozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai utakaofanyika Samarkand, Uzbekistan. Pia rais Xi atafanya ziara rasmi nchini Kazakhstan na Uzbekistan.