Rais wa China kuhudhuria mkutano wa SCO na kufanya ziara nchini Kazakhstan na Uzbekistan
2022-09-13 09:34:48| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying jana alisema, rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano wa 22 wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Samarkand, na kufanya ziara nchini Kazakhstan na Uzbekistan kuanzia tarehe 14 hadi 16 mwezi Septemba.

Hua amesema rais Xi Jinping atafanya ziara hizo kwa mwaliko wa mwenzake wa Jamhuri ya Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev na mwenzake wa Jamhuri ya Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev.