Rais anayemaliza muda wake wa Kenya Uhuru Kenyatta aahidi kupokezana madaraka kwa amani
2022-09-13 08:37:30| CRI

Rais anayemaliza muda wake nchini Kenya Uhuru Kenyatta alifanya mkutano jana Jumatatu na mrithi wake William Ruto, akisisitiza    nia yake ya kupokezana madaraka kwa amani nchini humo.

 

Kenyatta, ambaye baada ya mkutano wake na Ruto katika ikulu jijini Nairobi, alilihutubia taifa akitoa mkono wa kwaheri kupitia televisheni akisema atasimamia mchakato wa kupokezana madaraka leo Jumanne ili kuthibitisha tena upevu wa demokrasia nchini Kenya. Aidha Kenyatta alimpongeza Naibu wake Williamu Ruto kwa kushinda kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9 na kutoa wito wa kuunga   mkono serikali ijayo ambayo imedhamiria kuhudumia wananchi wote kwa usawa.

 

Katika  hafla ya kuapishwa itakayofanyika leo, Kenyatta atamkabidhi Ruto   alama za madaraka  zikiwemo upanga  na nakala ya katiba kuashiria mapokezano ya madaraka.