Kituo cha usalama dhidi ya virusi vya kompyuta cha taifa cha China chatoa ripoti kuhusu silaha ya mtandaoni ya “Suctionchar” ya Marekani
2022-09-13 18:22:37| cri
Leo Septemba 13, kituo cha taifa cha usalama dhidi ya virusi vya kompyuta cha China kimetoa ripoti kuhusu silaha ya mtandaoni ya “Suctionchar” ya Shirika la Usalama wa taifa la Marekani NSA.
Ripoti hiyo inasema kituo kicho kimegundua silaha maalumu ya mtandaoni iitwayo “Suctionchar” inayomilikiwa na Shirika la Usalama wa taifa la Marekani (NSA) kwenye seva ya mtandao ya Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kaskazini Magharibi(NUP) kilipochunguza shambulizi la mtandaoni dhidi ya Chuo Kikuu hicho. Uchambuzi wa kiufundi uliofanywa na kituo hicho kwa kushirikiana na kampuni ya usalama mtandaoni ya Qianxin, umedhihirisha kuwa silaha hiyo yenye uwezo wa kufanya udukuzi na kuiba siri, inalenga zaidi mfumo wa Unix/Linux, na kazi yake kuu ni kuiba nywila za akaunti ya ufikiaji wa mbali kwenye seva pangishi inayolengwa.