Rais mpya wa Kenya aahidi kuhimiza uhai wa uchumi na amani ya kikanda
2022-09-14 10:31:52| CRI

Rais mpya William Ruto wa Kenya jana alisema kuhimiza uhai wa uchumi, kubadilisha mfumo wa watumishi wa umma na kuhimiza mafungamano, biashara, amani na utulivu wa kikanda ni kazi kuu za serikali yake zitakazowekewa kipaumbele.

Muda mfupi baada ya Ruto kuapishwa kuwa rais wa tano wa Kenya mjini Nairobi alitoa hotuba rasmi akisema, atatumia siku zake za awali baada ya kuingia madarakani kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira na shinikizo la mfumuko wa bei yanayowakabili wananchi. Serikali yake itajitahidi kutoa nafasi za ajira na kuwanufaisha wananchi, na itachukua hatua ya kupunguza gharama ya maisha.

Ameongeza kuwa serikali yake imeshapanga kuwapatia wakulima mbolea na mbegu mnamo mwezi Oktoba katika msimu wa kupanda, ili kuongeza uzalishaji wa mazao makuu.