Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev
2022-09-14 23:17:29| cri

Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo ziarani nchini Kazakhstan leo amefanya mazungumzo na mwenzake wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev.

Kwenye mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa, hii ni ziara yake ya kwanza tangu kutokea kwa janga la COVID-19, ambayo inadhihirisha kiwango cha juu na upekee wa uhusiano kati ya China na Kazakhstan. Amesema serikali ya China inatilia maanani sana uhusiano wake na Kazakhstan, hata kama hali ya kimataifa itabadilika vipi, China siku zote inaiunga mkono Kazakhstan katika kulinda uhuru wa taifa na ukamilifu wa ardhi, kuunga mkono kithabiti hatua za mageuzi zake za kudumisha utulivu na maendeleo ya taifa, na kupinga uingiliaji wowote wa nje katika masuala ya ndani ya Kazakhstan. Ameongeza kuwa China daima ni rafiki na mshirika wa kuaminika wa Kazakhstan.