Ziara ya rais Xi yaonesha umuhimu mkubwa wa China kwenye SCO na uhusiano wake na Kazakhstan na Uzbekistan
2022-09-14 10:38:23| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning amesema, uwepo wa rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa 22 wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Samarkand, na ziara ya kiserikali nchini Kazakhstan na Uzbekistan itakayofanyika tarehe 14 hadi 16 mwezi Septemba, inaonesha umuhimu mkubwa wa China kwenye jumuiya ya SCO na uhusiano wake na nchi hizo mbili.

Bi. Mao amesema mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye mazingira ya kimataifa na janga la muda mrefu la UVIKO-19 yamesisitiza zaidi jukumu la SCO katika kusimamia usalama na utulivu wa kikanda na kukuza maendeleo na ustawi wa nchi. 

Mao amesema kwenye mkutano wa jumuiya ya SCO, rais Xi atabadilishana maoni kwa kina na viongozi wengine wanaoshiriki mkutano huo wakizingatia zaidi ushirikiano wa SCO wa pande zote na masuala makubwa ya kimataifa na kikanda ili kujenga maelewano ya pamoja na kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano.