Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China akutana na wabunge waandamizi wa Msumbiji na Burundi
2022-09-14 10:33:50| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Wang Yang amekutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Msumbiji Esperanca Bias na Spika wa Seneti ya Burundi Emmanuel Sinzohagera kupitia video.

Bw. Wang amesema kuwa China iko tayari kushirikiana na Msumbiji ili kuimarisha hali ya kuaminiana ya kisiasa, kuongeza mawasiliano ya kimkakati na kupanua ushirikiano kivitendo.

Kwa upande wake, Bibi Bias alisema kuwa urafiki na hali ya kuaminiana kati ya Msumbiji na China ni jambo lisiloweza kuvunjika ambapo nchi yake inaishukuru China kwa uungaji mkono na usaidizi wake thabiti na inatazamia ushirikiano wenye matunda zaidi kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Wang pia alikutana na Sinzohagera, ambapo amesema kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha hali ya kuaminiana ya kisiasa, kusaidiana kithabiti na kukuza ushirikiano kivitendo ili kupata matokeo zaidi chini ya mwongozo wa makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Sinzohagera amesema kuwa Burundi inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano na China. Na Burundi inashikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja na kupenda kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.