Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China yaonesha msimamo wa China wa kuongeza kiwango cha ufunguaji mlango
2022-09-14 20:27:46| cri

Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China yalifanyika tarehe 8 hadi tarehe 11 Septemba huko Xiamen, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. Kaulimbiu ya maonesho hayo ni "Maendeleo ya Dunia: Kushiriki Fursa za Kidigitali, Kuwekeza katika Wakati Ujao wa Kijani".

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema maonesho hayo yameonesha msimamo wa China wa kuongeza kiwango cha ufunguaji mlango kwa dunia.