Kongamano la ushirikiano wa vyombo vya habari la wenzi wa Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki lafanyika
2022-09-15 15:21:07| CRI

Kongamano la mwaka 2022 la ushirikiano wa vyombo vya habari la wenzi wa Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) pamoja na serikali ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, China, limefanyika mjini Nanning, na kushirikisha wajumbe karibu 180 kutoka zaidi ya vyombo 70 vya habari vya nchi 17.

Madhumuni ya kufanya kongamano hilo ni kuhimiza vyombo vya habari vya China na nchi wanachama wa Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki kufanya mazungumzo na ushirikiano kwa kina na upana zaidi, ili kuchangia ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya China na Umoja huo.