Rais Xi awasili Uzbekistan kwa ziara ya kiserikali na mkutano wa SCO
2022-09-15 09:41:53| CRI

Rais Xi Jinping wa China amewasili Samarkand Uzbekistan Jumatano jioni kwa ziara ya kiserikali na kuhudhuria mkutano wa 22 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO)

Akiwa uwanja wa ndege rais Xi alilakiwa na rais Shavkat Mirziyoyev, Waziri Mkuu Abdulla Aripov, Waziri wa Mambo ya Nje Vladmir Norov, Gavana wa jimbo la Samarkand Erkinjon Turdimov na viongozi wengine wa ngazi za juu.

Katika hotuba yake ya maandishi, rais Xi kwa niaba ya serikali na watu wa China, alitoa salamu zake za heri kwa serikali na watu wa Uzbekistan. Xi alisisitiza kuwa urafiki ulioanza kwa zaidi ya miaka elfu mbili kati ya China na Uzbekistan na watu wake bado una nguvu na uko hai. Ushirikiano wa kina na wa kimkakati kati ya nchi hizi mbili umechochea maendeleo ya kasi, na sio tu unanufaisha watu wa nchi mbili, bali pia unatoa msukumo mkubwa katika kuleta amani, utulivu, ustawi na maendeleo ya kanda.

Katika ziara hiyo rais Xi aliambatana na Ding Xuexiang, Yang Jiechi, Wang Yi, He Lifeng pamoja na wajumbe wengine wa msafara.