Watoto zaidi ya milioni 14 wachanjwa kwenye duru ya tatu ya kampeni ya chanjo za polio Tanzania
2022-09-15 09:37:50| CRI

Wizara ya Afya ya Tanzania jana ilisema watoto 14,690,597 chini ya umri wa miaka mitano walioko Tanzania Bara wamepata chanjo kwenye duru ya tatu ya kampeni ya chanjo za polio iliyoanzia tarehe 1 hadi 4 mwezi Septemba.

Waziri wa Afya wa Tanzania Bibi Ummy Mwalimu alitoa taarifa akisema, lengo la duru ya tatu ni kuwapatia chanjo za polio watoto 12,386,854, na kwa sasa watoto 14,690,597 wamepata chanjo, idadi ambayo ni asilimia 118.6 ya idadi iliyopangwa awali.

Ameongeza kuwa duru ya nne na ya mwisho ya chanjo za polio itafanyika mwezi Novemba mwaka 2022, na kuwashukuru wote wanaoshiriki kwenye kampeni hiyo ya kupata chanjo za polio wakiwemo wadau wa kimaendeleo.