China yaimarisha msingi wa ufufukaji wa uchumi kwa kutuliza biashara na nchi za nje na uwekezaji kutoka nchi za nje
2022-09-15 09:39:29| CRI

Mkutano wa baraza la serikali la China unaoendeshwa na Waziri mkuu Bw. Li Keqiang jana uliamua kuwa China itaendelea kuchukua hatua za kuimarisha biashara na nchi za nje na uwekezaji kutoka nje, ili kuimarisha msingi wa ufufukaji wa uchumi.

Mkutano huo unaeleza kuwa, kufungua mlango ni sera ya kimsingi ya China, biashara na nchi za nje zinaunga mkono ongezeko la biashara na nafasi za ajira, hivyo ni lazima kuongeza nguvu za kuimarisha biashara na nchi za nje na uwekezaji wa nje.

Mkutano huo pia umesisitiza kuwa, ni lazima kuunga mkono makampuni ili kuhakikisha oda zao na kupanua uwepo wao kwenye soko. Juhudi kubwa zaidi zitafanywa ili kuhakikisha utoaji wa nishati, nguvukazi na ugavu kwa kampuni za biashara za nje. Msaada kamili utatolewa kwa ajili ya mahitaji ili kuhakikisha utekelezaji wa mikataba.