“Mazungumzo ya Tiangong” na ndoto ya vijana wa Afrika kwa anga za juu
2022-09-15 14:46:42| CRI

Hujambo msikilizaji na karibu tena katika kipindi cha Daraja kinachokuletea masuala mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, na jinsi ushirikiano na uhusiano kati ya pande hizo unaimarisha urafiki wa jadi kati yao.

katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti itakayohusu ndoto za vijana wa Afrika kuhusu anga za juu, na pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi kuhusu mradi wa nishati endelevu wa Garissa uliojengwa na kampuni ya China nchini Kenya wasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa wakazi wa huko.