Rais wa China akutana na rais wa Uturuki
2022-09-16 15:08:18| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo huko Samarkand amekutana na mwenzake wa Uturuki Recep Erdogan.

Rais Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya China na Uturuki umedumisha mwelekeo mzuri, na ushirikiano wao halisi unaendelea kusukumwa mbele. Ameongeza kuwa ukweli umethibitisha kuwa, maendeleo ya uhusiano wa China na Uturuki yanalingana na maslahi ya muda mrefu ya nchi hizo mbili, na pia kuna maana muhimu kwa kukuza mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea.

Kwa upande wake, Rais Erdogan amesema uhusiano kati ya Uturuki na China unapiga hatua katika sekta mbalimbali, na nchi yake inapenda kuhimiza ushirikiano wake na China ikiwemo biashara na uwekezaji kupata mafanikio zaidi.