Marais wa China na Iran wakutana
2022-09-16 15:08:53| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China leo huko Samarkand amekutana na mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi.

Rais Xi amesema China na Iran zina urafiki wa jadi, na kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote ni chaguo la pamoja la nchi hizo mbili. Amesema China inapenda kuongeza mawasiliano na uratibu wa kimkakati na Iran, ili kuhimiza uhusiano wao kupata maendeleo mapya.

Naye Rais Raisi amesema, Iran inataka kuongeza kithabiti ushirikiano wa sekta mbalimbali na mawasiliano ya ngazi mbalimbali na China, na kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa, Iran itakuwa mwanachama rasmi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, hatua itakayosaidia Iran na China kuimarisha ushirikiano wao zaidi.