IGAD yaanzisha sera ya biashara ili kuongeza kasi ya mafungamano
2022-09-16 08:47:35| CRI

Shirika la Maendeleo ya Serikali za nchi za Afrika Mashariki (IGAD) jana lilianzisha sera ya biashara ili kuongeza kasi ya mafungamano ya kikanda.

Mkuu wa Tume ya IGAD nchini Kenya Fatuma Adan amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa sera ya biashara ya IGAD imeundwa ili kutoa nafasi ya uchumi wa kikanda iliyo wazi na ya umoja ambayo itapiga jeki biashara baina ya nchi za IGAD, kwa kuunda mazingira ya lazima na kuondoa vizuizi vya biashara kwa bidhaa na huduma.

Adan amesema sera ya biashara ya IGAD itatoa mfumo wa kupanua usafirishaji wa bidhaa ndani ya kanda kwa bidhaa za wanunuzi na bidhaa za mtaji kupitia maendelo ya minyororo ya thamani ya kikanda. Nchi za IGAD ni pamoja na Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan, Uganda, Eritrea na Sudan Kusini.