Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Pakistan
2022-09-16 15:09:25| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China leo huko Samarkand amekutana na waziri mkuu wa Pakistan Muhammad Shahbaz Sharif.

Rais Xi amesema China na Pakistan ni majirani na zina hatma ya pamoja, bila kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa, nchi hizo mbili ni wenzi wa kuaminiana wa kimkakati. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Pakistan kuhimiza uhusiano wao wa wenzi wa kimkakati kupata maendeleo zaidi, na kuharakisha kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya China na Pakistan katika zama mpya.

Naye waziri mkuu Shahbaz ameishukuru China kwa kutoa msaada kwa wakati kufuatia mafuriko yaliyotolea nchini Pakistan, na kuongeza kuwa Pakistan inapenda kushirikiana na China kuendeleza uhusiano wao kuwa na kiwango cha juu zaidi.