China yapinga vikali sheria ya Marekani inayohusu Taiwan
2022-09-16 08:50:37| CRI

Msemaji wa ofisi ya Baraza la serikali ya China inayoshughulikia mambo ya Taiwan Bibi Zhu Fenglian jana alilaani vikali ile inayoitwa “Sheria ya sera ya Taiwan mwaka 2022” lliyopitishwa na kamati ya uhusiano wa kidiplomasia ya baraza la juu la bunge la Marekani.

Zhu amesema kitendo cha kupitisha sheria hiyo ni ukiukaji mkubwa wa kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, pia kinakwenda kinyume na ahadi iliyotolewa na Marekani, na kuchokoza mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa China.

Zhu ameihimiza Marekani kusimamisha kauli na vitendo visivyo sahihi juu ya suala la Taiwan, kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, na kutekeleza ahadi iliyotolewa na serikali ya Marekani juu ya kutounga mkono nguvu za kutaka“Taiwan ijitenge na China”.