Rais Xi Jinping wa China atoa mwito wa kuimarisha ushirikiano wa kina, na kuendeleza moyo wa Shanghai
2022-09-16 19:18:09| cri

Rais Xi Jinping wa China amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kuiweka jumuiya hiyo kwenye njia sahihi, kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo na kiziinua zaidi nchi wanachama.

Rais Xi ameyasema hayo alipohudhuria vikao maalum kwenye mkutano wa 22 wa Baraza la Wakuu wa Nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Kwenye hotuba yake, Rais Xi ametoa wito kwa nchi wanachama kuendelea kujitolea kuhimiza moyo wa Shanghai, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kudumisha uhuru wa kimkakati na kulinda utulivu wa kikanda, kufuata ushirikishwaji na kunufaishana katika kuhimiza ushirikiano wa maendeleo, na kuendeleza mchakato wa upanuzi wa jumuiya hiyo na kuimarisha taasisi zake.