China na Russia kufanya Duru ya 17 ya Mazungumzo ya Kimkakati ya Usalama
2022-09-18 20:15:16| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning ametangaza kuwa, kutokana na mwaliko wa mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama Yang Jiechi, na mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni katibu wa Kamati ya Mambo ya Siasa na Sheria ya Kamati Kuu ya Chama Guo Shengkun, katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia Nikolai Patrushev atakuja China kuanzia tarehe 18 hadi 19 Septemba, na kuhudhuria Duru ya 17 ya Mazungumzo ya Kimkakati ya Usalama kati ya China na Russia na Mkutano wa Saba wa Utaratibu wa Ushirikiano wa Utekelezaji wa Usalama wa Sheria kati ya pande hizo mbili.