Somalia yatafuta ufadhili wa misaada ya ukame katika mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu
2022-09-19 08:53:30| CRI

Mjumbe maalum wa rais wa Somalia anayeshughulikia kukabiliana na ukame Abdirahman Abdishakur Warsame amesema, ukame nchini Somalia umekuwa mbaya sana na watu wapatao milioni 1, wakiwemo watoto, wanawake, na wazee, wamekimbia makazi yao kutokana na hali hiyo.

Akiongea na Shirika la habari la Xinhua kabla ya Kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Warsame amesema watu hawana chakula, maji huduma za afya, na wanakabiliwa na janga kubwa zaidi la kibinadamu katika miongo miwili iliyopita. Amebainisha kuwa wanakwenda kila mahali ili kupata msaada huo na kusaidia mamilioni ya Wasomali ambao wanateseka na maisha.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Pembe ya Afrika imekumbwa na njaa kali zaidi katika karne ya 21. Kwa miezi kadhaa, ukame unaosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ya viwango vya kihistoria, pamoja na mambo mengine, umesababisha uhaba mkubwa wa chakula katika nchi za Somalia, Ethiopia na Kenya.