Tarehe 17 September, ni Siku ya Usafi Duniani. Siku hii ni maalum kwa kukumbusha umuhimu wa usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko na ya kuambukiza. Usafi, uwe wa mazingira ama wa mwili, ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kukidumisha kwa ajili ya afya yake na jamii inayomzunguka. Suala la usafi limekuwa likitiliwa maanani sana na jamii katika sehemu mbalimbali duniani, lakini pamoja na kwamba suala hilo linatiliwa maanani, bado usafi wa mazingira ni jambo ambalo bado halijafuatiliwa inavyopaswa.
Katika kipindi hiki cha Ukumbi wa Wanawake tutazungumzia zaidi umuhimu wa maji na athari za kukosa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu.