Wang Yi afafanua maendeleo ya China na sera kuhusu Marekani
2022-09-20 19:27:22| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi huko New York amebadilishana maoni na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Uhusiano kati ya Marekani na China, Kamati ya Biashara kati ya Marekani na China, na Shirikisho la Wafanyabiashara la Marekani.

Kutokana na hali ya sintofahamu kuzidi kuongezeka katika mustakabali wa uhusiano kati ya China na Marekani, Wang ametoa ufafanuzi wa uhakika wa China katika pande tano, ambazo ni mustakabali wa maendeleo ya China, sera za China kwa Marekani, msimamo wa China wa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili, na nia ya China ya kufanya uratibu wa pande nyingi na Marekani.

Wang pia amesisitiza kuwa msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani lazima udumishwe vyema, hasa kanuni ya kuwepo kwa China moja.