Vikosi vya Somalia vyawaua wapiganaji 75 wa al-Shabab katikati ya nchi hiyo
2022-09-20 08:42:42| cri


 

Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Taifa la Somalia (SNA) Bw. Dowaa Yusuf Rageh jana amethibitisha kuwa, jeshi la nchi hiyo limewaua wapiganaji 75 wa kundi la al-Shabab kwenye opresheni iliyofanyika Jumapili mkoani Hiran, katikati ya nchi hiyo.

Bw. Yusuf amesema, opresheni ya kijeshi bado inaendelea, ambayo inalenga magaidi waliofanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali hivi karibuni.