Mkutano wa Baraza Kuu la UM wajadili njia za kufuata ili kuokoa malengo ya dunia
2022-09-20 08:43:11| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja huo Csaba Korosi wameungana na viongozi wa dunia na mabalozi wa heshima katika kutoa wito wa kuokoa Malengo ya Maendleo Endelevu (SDGs) na kurudi kwenye njia sahihi ya kujenga dunia bora ambayo haimuachi mtu nyuma.

Bw. Guterres ameitisha Kikao cha Tatu cha Muda wa Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa lengo la kuongeza kasi ya kutimiza ahadi ili kuhakikisha utekelezaji wa mafanikio wa Malengo ya Maendeleo Endelevu kutokana na muda wa kutimiza malengo hayo kuzidi kukaribia, na kutokana na wito wa masuluhisho ya kijasiri katika kutatua changamoto za dunia zinazoongezeka.

Naye Rais wa UNGA Bw. Korosi amerejea kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kusema, imekuwa kwa wakati na ni muhimu sana kurejea kwenye utekelezaji wa Malengo hayo kwa kuwa kasi ya utekelezaji wake imepungua. Ameongeza kuwa, huu ni wa wakati wa kuwa makini katika kuiokoa dunia, bila kujali athari nzuri na mbaya zitakazotokana na hatua hiyo, na pia amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutimiza ahadi zao walizotoa.