Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa mkutano wa viwanda na ugavi
2022-09-20 08:45:27| CRI

Rais wa China Xi Jinping ameutumia barua ya pongezi Mkutano wa Kimataifa wa Utulivu na Unyumbufu wa Mnyororo wa Viwanda na Ugavi unaoanza leo mjini Hangzhou, mkoa wa Zhejiang.

Katika barua yake, rais Xi amesema kudumisha unyumbufu na utulivu wa minyororo ya viwanda na ugavi duniani ni uhakikisho muhimu wa kuboresha maendeleo ya uchumi wa dunia, na kuhudumia maslahi ya watu duniani.

Amesisitiza kuwa China iko tayari kufanya kazi pamoja na nchi nyingine kwa kutumia fursa mpya zinazotokana na mapinduzi ya duru mpya ya  sayansi na teknolojia na mageuzi ya  viwanda, na kujenga mfumo wa dunia nzima wa mnyororo wa viwanda na mnyororo wa ugavi  uwe wa usalama na utulivu, wa uhakika na uwazi,  wa jumuishi na wa kunufaishana.