Mwakilishi maalumu wa rais wa China ahudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II
2022-09-20 19:25:50| CRI

Mwakilishi maalumu wa rais wa China ambaye pia ni makamu wa rais Wang Qishan amehudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II.

Wang aliwasilisha salamu za rambirambi za rais Xi Jinping na serikali na wananchi wa China kwa mfalme Charles III kutokana na kifo cha Malkia Elizabeth II, na kutoa salamu za pole kwa familia ya kifalme, serikali na wananchi wa Uingereza.

Mfalme Charles III alipokea salamu hizo na kusema, familia ya kifalme ya Uingereza inathamini sana urafiki na viongozi wa China, na kutilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya Uingereza na China, pia inatarajia kuendelea kufanya ushirikiano na China katika maendeleo endelevu na sekta nyingine katika siku zijazo.