China yasema idadi kubwa ya operesheni za kijeshi za Marekani katika nchi za nje yaonesha umwamba wake
2022-09-21 08:44:19| cri


 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana amesema, China imeona takwimu kuhusu operesheni za kijeshi zilizofanywa na Marekani katika nchi za nje, ambazo zimeonyesha umwamba wa Marekani.

Amesema Marekani hutangaza “kuheshimu na kulinda utaratibu wa kimataifa kwa msingi wa kanuni”, lakini takwimu hizo zimeonesha ukweli wa nchi hiyo kupenda vita na umwamba wa kanuni za Marekani.

Takwimu zilizotolewa na Idara ya Huduma ya Utafiti wa Bunge la Marekani zimeonyesha kuwa, kuanzia mwaka 1798 hadi 2022, Marekani ilifanya operesheni 469 za uingiliaji wa kijeshi katika nchi za nje.