CIIE yaanza kuandikisha waandishi wa habari
2022-09-21 10:06:16| CRI

Waandishi wa habari watakaoshiriki katika Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Bidhaa Zinazoagizwa na China Kutoka Nchi za Nje (CIIE) yatakayofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 10 mwezi Novemba mjini Shanghai wameanza kujiandikisha leo.

Waandishi hao wanatakiwa kujiandikisha kuanzia leo tarehe 21, Septemba hadi tarehe 10, Oktoba kupitia tovuti ya www.ciie.org au APP ya simu ya mkononi.

Kutokana na hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi, waandishi wanaoruhusiwa kujiandikisha ni wale wanaotoka China bara, Hong Kong, Macao, Taiwan, na nchi za nje ambao wako nchini China.