Idadi ya vifo kutokana na ajali ya boti nchini Nigeria yafikia 11
2022-09-21 08:38:12| cri

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya boti iliyotokea jumamosi iliyopita katika Jimbo la Yobe, kaskazini magharibi mwa Nigeria, imeongezeka na kufikia 11.

Msemaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mambo ya Dharura katika mkoa huo Bw. Mohammed Goje, amesema miili 11 ilipatikana kaika operesheni ya uokoaji inayoendelea katika eneo la Jumbam, wilaya ya Tarmuwa.

Bw. Goje alisema, watu wanane waliojeruhiwa wameokolewa na kupewa matibabu katika hospitali ya eneo hilo.