Uchumi wa Afrika wakabiliwa na tishio la mgogoro wa hali ya hewa na mashaka juu ya kanuni
2022-09-21 08:41:14| CRI

Wataalam wa Afrika wamesema, mgogoro wa hali ya hewa na wasiwasi wa kisiasa na kanuni vinatishia ukuaji endelevu wa uchumi wa Afrika.

Wakizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2022 ya Alama za Hatari na Faida za Uchumi wa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao, wataalam hao wamesema bara hilo linapaswa kukabiliana na matishio yanayoibuka ya mapigano, mgogoro wa hali ya hewa, na wasiwasi wa kisiasa na kanuni ili kudumisha ukuaji wa uchumi.

Ripoti hiyo imesema, ukuaji wa baadaye wa Afrika utategemea zaidi katika matumizi ya nishati mpya, uwekezaji katika mfumo wa chakula unaovumilia mabadiliko ya hali ya hewa, kuongeza kasi ya maingiliano, na usimamizi mzuri wa fedha za umma.

Mchambuzi mwandamizi katika Kituo cha Kudhibiti Hatari cha Afrika Magharibi, Patricia Rodrigues amesema, nia ya Afrika ya ufufuaji wa uchumi iko hatarini kutokana na vurugu zinazohusiana na janga la COVID-19, vita kati ya Ukraine na Russia, na ukame unaoendelea.