Mkuu wa UM atoa wito wa kutoa msaada wa fedha ili kukabiliana na njaa kwenye Pembe ya Afrika
2022-09-22 08:58:33| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kutoa msaada wa fedha kwa ajili ya shughuli zote za msaada kwenye Pembe ya Afrika kutokana na kanda hiyo kukabiliwa na njaa inayosababishwa na ukame.

Guterres amesema mamilioni ya watu katika nchi za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya na Somalia wanakabiliwa na ukame mbaya zaidi kutokea karibu nusu karne iliyopita.

Wasaidizi wa kibinadamu walioko huko wameeleza kuwa, watoto wengi wanakabiliwa na utapiamlo mkali, mamilioni ya wanyama wamekufa kando ya mashamba yasiyo na matunda, na bei za vyakula ziko juu.

Guterres amesema ni vigumu kusisitiza ukali wa maafa yanayotokea, lakini hatua zikichukuliwa mapema, hali mbaya zaidi itaweza kuzuiliwa.