Rais wa China atoa barua ya pongezi kwa maadhimisho ya Siku ya Amani ya Kimataifa
2022-09-22 08:54:32| cri

Shughuli ya Maadhimisho ya Siku ya Amani ya Kimataifa ya mwaka 2022 zilifanyika Beijing jana Tarehe 21 Septemba, Rais wa China Xi Jinping  alitoa barua ya pongezi  kwa shughuli hiyo. 

Katika barua yake, Rais Xi amesema kauli mbiu ya  shughuli ya maadhimisho ya Siku hiyo ya mwaka huu ni “kutekeleza pendekezo la usalama wa dunia na kulinda amani na utulivu wa dunia”, hii inafuata moyo wa katiba ya Umoja wa Mataifa  wa kulinda amani na usalama wa kimataifa. Alitumai kuwa shughuli hiyo ya maadhimisho    inakusanya akili na nguvu za pande mbalimbali, ili  kutoa mchango wa hamasa kwa ajili ya kulinda amani na utulivu wa dunia.