Kuchagua njia sahihi ya kuzuia mimba kutasaidia afya ya wanawake
2022-09-23 13:15:21| CRI

Tarehe 26 Septemba kila mwaka ni SIku ya Kimataifa ya Kuzuia Mimba (World Contraception Day). Kampeni kubwa katika siku hii ni kuhakikisha kuwa, mwanamke anakuwa mjamzito kwa matakwa yake. Siku hii ambayo ilizinduliwa rasmi mwaka 2007, ina lengo la kuboresha uelewa wa njia za kuzuia mimba na kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yao ya uzazi na kujamiiana.

Katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake tunazungumzia suala la uzazi wa mpango na njia za kuzuia mimba.