UM watoa wito wa hatua za kiujenzi kukabili matatizo katika kanda ya Sahel
2022-09-23 08:44:12| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa hatua za kiujenzi ili kukabiliana na matatizo yanayolikumba eneo la Sahel.

Akizungumza kando ya Mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo jana, Bw. Guterres amesema mgogoro wa usalama katika kanda ya Sahel ni tishio kwa dunia, na kama hakuna hatua zitakazochukuliwa, athari za ugaidi, msimamo mkali na uhalifu wa kupangwa zitavuka mpaka wa eneo hilo na bara la Afrika.

Amesema kama sehemu za juhudi za kukabiliana na hali hiyo, Jopo Huru la Ngazi ya Juu litaundwa, likiongozwa na aliyekuwa rais wa Nigeria Mahamadou Issoufou, na litafanya tathmini huru na kutoa mapendekezo halisi ili kukabiliana na changamoto hizo na kukusanya rasilimali zinazotakiwa ili kupata suluhisho la kudumu la changamoto hizo.