Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Somalia wakutana
2022-09-23 08:42:49| CRI


 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na mwenzake wa Somalia Abshir Omar Huruse jijini New York, Marekani.

Wang amesema, urafiki wa jadi kati ya China na Somalia ni sehemu muhimu ya urafiki kati ya China na Afrika, na Somalia ni nchi ya kwanza ya Afrika Mashariki iliyoanzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China. Ameongeza kuwa nchi hizo mbili daima zinaheshimiana na kusaidiana katika masuala yanayohusu maslahi ya kimsingi.

Wang amesisitiza kuwa China daima inatetea kwamba nchi zote ni sawa, bila kujali ni kubwa au ndogo, yenye nguvu au kuwa dhaifu, ni tajiri au maskini.

Kwa upande wake, Huruse amesema Somalia inafurahia urafiki wa muda mrefu na China, na inaishukuru kwa dhati China kwa kuisaidia Somalia katika nyakati ngumu, hasa kwa kuiunga mkono Somalia katika kulinda mamlaka yake ya nchi.