Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria na kuhutubia mjadala wa mkutnao wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa
2022-09-26 08:39:36| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi Jumamosi alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kila juhudi kwa ajili ya amani na maendeleo, na kubeba jukumu la kuhimiza mshikamano na maendeleo.

Akihutubia mjadala wa jumla wa  Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa, Bw. Wang Yi amesema dunia imeingia kwenye kipindi kipya cha mitikisiko na mabadiliko ambayo hayajashuhudiwa katika karne iliyopita, hata hivyo amani na maendeleo bado vinaendelea kuwa mwelekeo wa zama hizi, huku sauti za watu wa sehemu mbalimbali duniani za kutaka maendeleo na ushirikiano zikiongezeka. 

Bw. Wang amesema jibu la China kuhusu namna ya kuitikia wito wa zama na kufuata mwelekeo wa kihistoria wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja liko thabiti na wazi, kama ilivyopendekezwa na Rais Xi Jinping wa China.