Misri yatuma msaada Somalia, na kuwahamisha wanajeshi waliojeruhiwa katika mashambulizi ya kigaidi
2022-09-26 09:14:19| CRI

Misri imetuma ndege mbili za kijeshi zilizobeba vifaa vya misaada kwa Somalia kufuatia amri ya rais Abdel Fattah el-Sisi.

Ikulu ya Misri imesema msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia kupunguza shinikizo linalobebwa na watu wa Somalia.

Licha ya hayo, Misri pia imetuma timu mbili za kutoa huduma ya matibabu kusaidia kuwahamisha wanajeshi wa Somalia waliojeruhiwa katika mashambulizi ya kigaidi na kuwafikisha katika hospitali za jeshi la Misri.   

Taarifa pia imesema idara ya huduma za matibabu ya Misri imeinua kiwango cha tahadhari katika hospitali hizo mara moja ili kutoa matibabu kamili kwa wanajeshi hao waliojeruhiwa.