UM watoa wito kwa Mali kuwaachilia askari wa Cote d’Ivoire wanaoshikiliwa
2022-09-27 08:45:44| CRI

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi mkubwa juu ya kuendelea kushikiliwa kwa askari wa Cote d’Ivoire nchini Mali na kutoa wito wa askari hao kuachiliwa.

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema sekritarieti ya Umoja wa Mataifa inatoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa askari wa Cote d’Ivoire kwa kufuata moyo wa undugu kati ya Cote d’Ivoire na Mali.

Msemaji huyo amesema Umoja wa Mataifa unaunga mkono juhudi zote za kuwezesha kuachiliwa kwa askari waliokamatwa mjini Bamako Julai 10. Umoja huo pia umesisitiza uungaji mkono wa “kurejeshwa kwa amani na kuhimiza ujirani mwema kati ya nchi hizo mbili”.

Kabla ya hapo Mali iliwashutumu askari wa Cote d’Ivoire kuwa mamluki na kusimamisha mizunguko yote ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa.