Nchi karibu 70 zasisitiza kutoingilia mambo ya ndani ya China
2022-09-27 09:37:16| CRI

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Pakistan kwa niaba ya nchi 68 Jumatatu wiki hii kwenye mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, imesisitiza kuwa masuala yanayohusu Xinjiang, Hong Kong na Tibet ni mambo ya ndani ya China, na suala la haki za binadamu halitakiwi kutumiwa kwa malengo ya kisiasa na kuweka vigezo viwili au kuingilia mambo hayo kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Taarifa hiyo imesema kuheshimu mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi huru ni kanuni za msingi zinazoongoza mahusiano ya kimataifa. Pande zote zinatakiwa kuzingatia na kufuata malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kuheshimu haki ya kila nchi kuchagua njia yake ya maendeleo.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kuwa haki zote za binadamu zikiwemo haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni haswa haki za maendeleo zinatakiwa kuwa na msisitizo sawa.