Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wafungwa mjini New York
2022-09-27 09:05:15| CRI

Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefungwa mjini New York, baada ya wawakilishi wa nchi 190 wanachama kutoa hotuba kwenye mkutano huo.

Kwenye ufungaji wa mkutano huo, mwenyekiti wa mkutano huo Bw Csaba Korosi amesema wakuu wa nchi na serikali wapatao 126 walishiriki kwenye mkutano wa mwaka huu, hali inayoonesha umuhimu wa mkutano huo kwenye mambo ya kimataifa.

Amesema kwenye mkutano huo mambo matano yamejulikana, ikiwa ni pamoja na kuwa dunia imeingia kwenye zama mpya, mgogoro wa Ukraine unatakiwa kumalizika, na kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanaharibu dunia.