Rais Xi aandika dibaji kwa mkusanyiko wa fasihi kuhusu ustawishwaji wa taifa
2022-09-27 08:46:26| CRI

Rais Xi Jinping wa China ameandika dibaji yenye kichwa cha “Kusonga Mbele Kuelekea Ustawishwaji wa Taifa”, kwa ajili ya mkusanyiko wa fasihi kwenye Maktaba ya Ustawishwaji, ambao unatarajiwa kuchapishwa hivi karibuni.

Kwenye dibaji hiyo Rais Xi amesisitiza haja ya kujifunza kutokana na historia, kutupia macho siku za baadaye, na kusonga mbele kwenye safari ya kutimiza ustawishwaji wa taifa.

Rais Xi amesema, mkusanyiko huo wa vitabu uitwao “Maktaba ya Ustawishwaji” ni mradi mkubwa wa kiutamaduni ulioidhinishwa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kuchapishwa kwake ni muhimu kwa watu wa China kuwa na imani na historia, kushikilia mwelekeo wa zamu, kufuata njia ya China, na kusukuma mbele ustawishwaji wa taifa kupitia njia ya China kuelekea kuwa nchi ya kisasa.