Madaktari wa China waleta mageuzi ya tiba ya Gastroscopy na matibabu ya Kichina nchini Sudan Kusini
2022-09-28 08:56:13| CRI

Kikundi cha 10 cha madaktari wa China nchini Sudan Kusini kimeanzisha mbinu mpya ya matibabu, inayounganisha matumizi ya Gastroscopy na tiba ya akyupancha kuwapunguzia maumivu wagonjwa Sudan Kusini.

Madaktari wa China walioko kati hospitali ya mafunzo ya Juba, walipendekeza matumizi ya njia hiyo kwa mgonjwa mmoja aliyekwenda kwenye hospitali hiyo. Madaktari walimfanyia upimaji mgonjwa huyo na kufanikiwa kugundua uvimbe tumboni, na kupelekwa kwenye chumba cha upasuaji kwa matibabu zaidi.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa njia hiyo kutumiwa kwenye matibabu nchini Sudan Kusini.